Mkurugenzi wa label ya MDB ambayo inamsimamia msanii Young Dee, Max Rioba, anasema tayari wao kama uongozi unaandaa mpango maalum ambao utampa fursa rapa huyo ya kuwaelimisha vijana kuhusu athari za matumizi ya Madawa ya kulevya.
Rapper Young Dee aka ‘rapa paka’ baada siku ya jana kukiri alikuwa anatumia Madawa na kulevya, ana mpango maalum ambao utaweza kuelimisha vijana kuhusu athari za matumizi ya Madawa ya kulevya.
“Tuna project ambayo tunaifanyiakazi, ambayo ziwezi kuiweka wazi zaidi kwa sababu ni mapema,” alisema Max.
“Nina uhakika utakapofikia wakati wake yeyote yule ambaye anataka kuingia kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya atajiuliza mara mbilimbili, sisi tulimuonyesha Young Dee wasanii ambao wameathirika na Madawa ya kulevya, tukamuuliza unataka kuwa kama fulani? Ungependa kesho tuwe na press conference kwamba umekufa? Kwamba tulikuwa na msanii, kwa hiyo kupitia mtindo kama huu utabadili mawazo ya vijana wengi”
Rapa huyo alikiri kutumia Madawa ya kulevya kwa kipindi cha mwaka mmoja.
0 comments :
Post a Comment