HISPANIA IMEWEKA REKODI MPYA ULAYA BAADA YA KUICHAPA JAMHURI YA CZECH


Hispania imeanza vizuri kampeni za kutwaa taji la mataifa ya Ulaya kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuichapa Jamhuri ya Czech.
Bao la kichwa la dakika za lala salama lilofungwa na mlinzi Gerard Pique akiunganisha krosi ya Andres Iniesta hatimaye lilipeleka faraja kwa wahispania kufuatia upinzani mkali walioupata kutoka kwa wapinzani wao.
Alvaro Morata, Jordi Alba na David Silva juhudi zao ziligonga mwamba huku mabingwa hao watetezi wa taji la Ulaya wakishindwa kufunga katika dakika za mapema na kusubiri hadi dakika za jioni.
Hispania pia ilinurusika kuchapwa bao pale Cesc Fabregas alipookoa mpira kwenye mstari wa goli uliopigwa na Theodor Gebre Selassie
Vladimir Darida alipata nafasi ya kuisawazishia Jamhuri ya Czech lakini mlinda mlango wa Hispania David de Gea alikuwa vizuri langoni licha ya tuhuma zinazomkabili.
Rekodi zilizowekwa baada ya mchezo wa Hispania dhidi ya Jamhuri ya Czech
  • Hispania sasa haijapoteza mchezo wowote kati ya michezo 13 iliyopita kwenye fainali za Euro tangu walipofungwa na Ureno mwaka 2004.
  • Kikosi cha mabingwa hao watetezi wa kombe la mataifa ya Ulaya hawajaruhusu goli ndani ya dakika 600 zilizopita kwenye michuano ya Ulaya, kipindi kirefu zaidi kutokea kwenye mashindano hayo.
  • Golikipa wa Jamhuri ya Czech Petr Cech ndiye mchezaji pekee aliyepiga pasi nyingi zaidi kwenye mchezo dhidi ya Hispania kuliko mchezaji yeyote kwenye timu hiyo, Cech amepiga pasi 36.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment