VILABU VYA IRELAND NA VIMBAUMBAU WA UTURUKI: TAKWIMU ZOTE KALI ZA EURO 2016 HIZI HAPA!


Asalam Aleykum iwe ni salamu yangu ya upendo na heri njema kwa wataalamu wangu wote mnaopenda kupata habari na takwimu bomba za kimichezo.
Msimu wa soka la kitabu na magoli yanayofanyiwa homework kabla ya mechi kuanza ndio umewadia.
EURO20 16 ndio michuano pekee inayotupatia ladha halisi ya soka la kileo zaidi ya michuano yoyote ile Ulimwenguni. Kabumbu lenye misingi ya academy, uchambuzi wa kila takwimu ya timu pinzani, na uweledi wa juu kabisa katika kuunganisha teknolojia sambamba na ufundi uwanjani.
Hili ndiyo soka la kisasa, ndiyo maana haishangazi kuona katika mechi tatu fainali za kombe la Dunia zilizopita, timu tano(5) zikitokea barani Ulaya (Germany, Hispania, Uholanzi, Italia na Ufaransa) na timu moja pekee kutoka shirikisho la Amerika kusini (Argentina)!
Wakati mashabiki wakielekeza akili zao kwenye kushuhudia ufundi wa soka linavyotandazwa kwenye nyasi za pale France, zifuatazo ni takwimu za kusisimua na kuongeza hamasa miongoni mwa wafuatiliaji wake:-
a.) Wachezaji Makinda Zaidi
  1. Marcus Rashford (England) – miaka 18, siku 146.
  2. Renato Sanches (Portugal) – miaka 18, siku 218.
  3. Emre Mor (Turkey), miaka 18, siku 261
b.) Wachezaji Wakongwe Zaidi
  1. Gábor Király (Hungary) – mlinda mlango huyu alizaliwa 01/04/1976, hivyo siku ya Juni 14 atakaposhuka dimbani kukwaana na timu ya Austria atakuwa na umri miaka 40 na siku 74. Na hii itaashiria kuvunjwa kwa rekodi inayoshikiliwa na nguli wa kijerumani Lothar
    Matthäus alipocheza akiwa na umri wa miaka 39, siku 91 katika mchezo wa Euro 2000 dhidi ya Portugal katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi.
c.) Vikosi Vyenye Wastani Mdogo Zaidi Wa Umri
  1. England – 25, siku 39.
  2. Germany – 25, siku 44.
  3. Switzerland/Uswisi – 25, siku 51.
d.) Vikosi Vyenye Wastani wa Umri Mkubwa Zaidi
  1. Jamhuri ya Ireland – 29, siku 3.
  2. Russia 28, siku 83.
  3. Jamhuri ya Czech Republic – 28, siku 70.
e.) Wachezaji Warefu Zaidi
  1. Costel Pantimillion – 2.03 m (Romania, golikipa)
  2. Fraser Forster – 2.01m (England, Golikipa)
  3. Lovre Kalinić – 2.01 (Croatia, Golikipa)
f.) Wachezaji Wafupi Zaidi
Ulikuwa unafikiri wachezaji wa kimo cha ‘anko’ Ngassa wapo kwenye Ndondo Cup pekee, umekosea….
  1. Lorenzo Insigne – 1.63m (Italy)
  2. Jamie Ward – 1.65m (Northern Ireland, MF)
  3. Pedro Rodríguez – 1.67m (Spain)
g.) Wastani wa Urefu wa Kila Kikosi
  1. Sweden 1.86m (Sweden)
  2. Austria, Belgium, Croatia, Germany, Hungary, Iceland – 1.85m
  3. Jamhuri ya Czech, Poland, Slovakia, Switzerland, Ukraine – 1.84m
  4. England, Italy, Ireland Kaskazini, Jamhuri ya Ireland, Russia – 1.83m
  5. Albania, France, Romania – 1.82m
  6. Portugal, Turkey, Wales – 1.81m
  7. Spain – 1.80m
h.) Wastani wa Uzito wa Kila Kikosi
  1. Germany – 80.30kg
  2. Sweden – 80.17kg
  3. Switzerland – 79.70kg
  4. Hungary – 79.43kg
  5. Austria – 79.17kg
  6. Croatia – 78.87kg
  7. Iceland – 78.52kg
  8. Jamhuri ya Czech – 78.35kg
  9. Belgium – 77.78kg
  10. Poland – 77.74kg
  11. Jamhuri ya Ireland – 77.70kg
  12. Slovakia – 77.70 kg
  13. Russia – 77.48kg
  14. Italy – 77.00kg
  15. Ufaransa – 76.91kg
  16. Ireland Kaskazini – 76.78kg
  17. Romania – 76.09kg
  18. Wales – 75.70kg
  19. Albania – 75.65kg
  20. Portugal – 75.61kg
  21. Ukraine – 75.35kg
  22. England – 75.17kg
  23. Spain – 74.35kg
  24. Uturuki – 74.30kg
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment