Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetangaza majina ya waamuzi watakaochezesha mashindano ya kombe la shirikisho Afrika kwa hatua ya makundi yanayotarajiwa kutimua vumbi wiki ijayo.
Tanzania ikiwakilishwa na Yanga, inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi Juni 19 na timu Mouloudia Olimpique Bejaia kutoka Algeria, huku mchezo huo ukichezeshwa na mwamuzi kutoka nchini Morocco [Bouchaib El Ahrach] akisaidiwa na washika vibendera, Redouane Achik na Youssef Mabbrouk.
Aidha baada ya mchezo huo timu ya Yanga inatarajiwa kukutana na timu ya TP Mazembe Juni 28 mchezo utakaochezwa uwanja mkuu wa taifa huku mchezo huo ukiongozwa na mwamuzi, Janny Emiliano (Zambia) pamoja na washika vibendera wake Jerson Emiliano (Angola) na Berhe O’michael (Eritrea).
Timu nyingine zitakazocheza mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ni pamoja na MO Bejaia (Algeria) vs Esperance (Tunisia), Stade Malien (Mali) vs FUS Rabat (Morocco), Etoile du Sahel (Tunisia) vs CF Mounana (Gabon), TP Mazembe (DR Congo) vs Stade Gabesien (Tunisia), Ahli Tripoli (Libya) vs Misr Makassa (Egypt), El Merreikh (Sudan) vs Kawkab (Morocco), Young Africans (Tanzania) vs Sagrada Esperanca (Angola), Mamelodi Sundowns (South Africa) vs Medeama (Ghana).
0 comments :
Post a Comment