SIMBA NI NJIA YANGU NYINGINE, MNYATE


Kiungo mshambulizi wa zamani wa timu za Taifa za Vijana na klabu za Burkina Faso, Azam FC, Mtibwa Sugar na Mwadui FC, Jamali Simba Mnyate amesema ameamua kuichagua Simba SC na kusaini mkataba wa miaka miwili ili kujiendeleza kimpira na kufanya kazi bora ili kuinyanyua timu hiyo iliyopoteza mwelekeo kwa misimu minne mfululizo.
“Nimefurahi kusajiliwa na Simba”, anasema Mnyate katika mahojiano mafupi niliyofanya naye siku ya leo Jumatatu akiwa mkoani Morogoro.
“Nimesaini mkataba wa miaka miwili. Unajua kila mtu huwa na ndoto zake nami kama mchezaji nilikuwa na ndoto ya kuichezea klabu kubwa katika nchi na Simba ni mojawapo ya timu kubwa nchini”, anasema Mnyate aliyezaliwa August 7, 1992, Kilosa, Morogoro.
“Si kwamba nimefika mwisho wa mafanikio kisoka baada ya kufika hapa, Simba ni njia nzuri za mchezaji kufikia mafanikio ya kuwa mchezaji wa kulipwa. Nilikuwa na ndoto ya kuichezea klabu kubwa. Nawaahidi mashabiki wa timu yangu mpya kujitolea ili kuisaidia Simba kufanya vizuri msimu ujao. Naomba tushirikiane kwa pamoja, tutafanikiwa.”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment