Chama cha wananchi CUF kinazidi kuleta mapya kutokana na mambo kadha wa kadha yanayokuwa yakitokea. Jana viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
wamekutana kujadili mgogoro wa CUF sababu ni moja ya vyama vinavyounda
UKAWA.
Viongozi wa UKAWA jana wametangaza kuwa hawamtambui Prof. Lipumba kama mwenyekiti wa CUF na kuwa wao watashirikiana na viongozi halali wa CUF, na kutilia maanani maazimio yaliy0pitishwa katika vikao halali vya CUF.
Aidha,
mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amewataka viongozi wa chama hicho
nchini kote kumpuuza na kutompa ushirikiano Prof. Lipumba kwani ni
msaliti.
Kwa upande wake yeye, Prof. Lipumba ameendelea kutekekelza majukumu yake kama Mwenyekiti wa CUF ambapo jana ametangaza kutengua uteuzi wa Wakurugenzi na Manaibu Wakurugenzi wa Idara mbalimbali za Chama cha Wananchi (CUF).
Wakurugenzi na Manaibu Wakurugenzi ambao uteuzi wao umetenguliwa ni pamoja na;-

- Joran Bashange – Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha
- Ismail Jussa- Mkurugenzi wa Mambo ya Nje
- Mustafa Wandwi- Mkurugenzi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama
- Kurufumu Mchuchuli- Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria
- Shaweji Mketo- Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi na
- Abdalla Mtolea- Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje
Aidha Prof. Lipumba amesema kuwa hajali kama viongozi wa UKAWA wanamtaka au hawamtaki kwani yeye anachojali ni kuijenga CUF.
0 comments :
Post a Comment