Wajumbe wa bodi chama cha wananchi CUF, wanaandaa utaratibu wa kuwakutanisha katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif na mwenyekiti wake, Prof.Ibrahim Lipumba ili kuwapatanisha kutokana na mgogoro ulioibuka na ambao unaendelea kukigawa chama hicho.
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wajumbe hao wa CUF wanne kati ya watano kutoka Tanzania bara wamesema wanahuzunishwa na mgogoro ndani ya chama hicho.
Mjumbe wa bodi CUF,Peter Malebo ameeleza kuwa watawaita viongozi hao makao makuu ili waweze kupata suluhu na kumaliza mgogoo huo unao endelea.
“Ndio maana wenzetu wamekaaa Zanzibar kwa kurubuniwa wale wajumbe wa bodi,na sisi tumekaa hapa ilA sasa viongozi wetu wakuu tumuombe Maalif Seif pamoja na Profesa Lipumba,tutawaita waje hapa makao makuu na wajumbe wote wabodi tukae nao tumalize mgogoro wetu,” aliomba Malebo.
Hivi karibuni, baraza la uongozi la chama cha Wananchi (CUF), lilitangaza kumfukuza uanachama Lipumba. Alifukuzwa kwa kile kilichoelezwa kuwa amekwenda kinyume na katiba ya chama na kufanya uasi kwa wanachama.
0 comments :
Post a Comment