AUDIO: Mtoto kutupwa mkoani Iringa asubuhi ya la leo tarehe 2 Oktoba, 2016

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhHbkHxEsMXagC3wJj6E2-UqXd9bELYjbCsXEkdki5SqTVbJ_l-INlQjofNB9kbcfKgitpvOLTGMDfMrKwfSUvjP1jtVRG5Sw6O9vB-QCi6ucaY4hN5JPhY_cwY-gV-pdyoinJQvaerxJf9/s640/18.jpg

Mtoto mchanga anayesadikika kuwa na umri wa miezi saba ambaye jinsia yake haikufahamika amekutwa akiwa ametupwa katika dampo la takataka katika eneo la njiapanda ya Kwa Beda mtaa wa Mwenge katika kata ya Kihesa mkoani Iringa siku ya leo tarehe Oktoba majira ya asubuhi.
Akiongea na Nuru fm shuhuda wa tukio hilo aliyefahamika kwa jina moja la Diana ameeleza kuwa baada baada ya kwenda kumwaga taka katika eneo hilo ndipo aliweza kubaini mwili wa mtoto huyo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mwenge Bi Helena Msilu amesema kuwa tayari askari wamefika eneo la tukio na kumchukua motto kwa uchunguzi zaidi na kwamba tukio hilo ni la kwanza kutokea mtaani hapo.

Bi Msilu ametoa wito kwa watu wanaofanya vitendo kama hivyo kuacha mara moja kabla hawajachukuliwa hatua kali za kisheria na watu watoe taarifa mara moja pindi wanapoona vitendo kama hivi vinatokea.

Endelea kufuatilia blog hii kwa taarifa zaidi........

RIPOTI KAMILI NI HII HAPA KUTOKA KWA DENIS NYALI KUPITIA NURU FM....
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment