Mkuu wa wilaya ya Geit Herman Kapufi amewataka askari wa
usalama barabarani kusimamia kikamilifu watumiaji wa barabara kwa kuwa wana
dhamana ya kusimamia sheria na kuwachukulia hatua wanaovunja sheria za usalama
barabarani.
Kapufi ameyasema hayo siku ya kilele cha maadhimisho ya
siku ya nenda kwa usalama barabarani ambapo kitaifa imeadhimishwa mkoani Geita
huku wakikumbushwa kutunza alama za barabarani.
Naye katibu wa baraza la taifa la usalama barabarani
ambaye pia ni kamanda wa polisi wa kikosi cha usalama barabarani Mohammed
Mpinge, amesema jeshi hilo limetoa elimu ya usalama wa barabarani kwa makundi
tofauti tofauti mkoani Geita.
Maadhimisho ya siku ya usalama barabarani yalianza siku
ya tarehe 26 ya mwezi Septemba mwaka huu na hivi leo ni kilele cha maadhimisho
hayo yenye kaluli mbiu isemayo Hatutaki ajali tunataka kuishi salama.
0 comments :
Post a Comment