Leo klabu ya Man United
walazimishwa sare ya 1-1 katika uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Stoke
City, mchezo uliofuatia ulikuwa ni wa Tottenham Hotspur dhidi ya Man
City katika uwanja wa White Hatlane.
Kama ambavyo wengi walitarajia kuona Man City akiodoka n ushindi
kutokana na rekodi yake msimu huu wa kucheza mechi sita EPL na kushinda
zote, ndivyo Tottenham walivyokuwa wamejipanga na kudhamiria kuvunja
ubabe wa Man City na kuwafanya wabaki kuwa klabu pekee msimu huu
haijapoteza mchezo.
Tottenham ambao nao hawajafungwa mchezo wowote msimu wakiwa wameishia
kutoka sare mechi mbili, wamefanikiwa kuifunga Man City goli 2-0, magoli
ambayo Man City walijifunga dakika ya 9 kupitia mchezaji wao Aleksander
Korarov na baadae Dele Allia akafunga goli la pili dakika ya 37 baada
ya kutumia vyema pasi ya Son Heung-Min, Spurs walipata penati dakika ya
lakini golikipa wa Man City Claudio Bravo alifanikiwa kuokoa shuti la
Lamela.
0 comments :
Post a Comment