Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameteua wakurugenzi wapya pamoja na manaibu wakurugenzi ndani ya chama hicho ikiwa ni siku moja tu baada ya kutengua wakurugenzi ndani ya chama hicho.
Akitangaza wakurugenzi wapya mbele ya waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho Buguruni Jijini Dar Es Salaam, Profesa Lipumba amemteua Thomas Malima kuwa mkurugenzi wa uchumi na fedha, Maftaha Chuma Mkurugenzi wa mambo ya nje, Zainab Ndorwa Mkurugenzi wa haki za binadamu na sheria.
Wengine walioteuliwa ni pamoja na Masoud Mhina katibu kamati ya ulinzi na usalama, Japhary Mnete Naibu Mkurugenzi wa mipango na uchaguzi, ambapo wakurugenzi na manaibu wakurugenzi waliochaguliwa baada ya mkutano wa June, 2014 wataendelea na nyadhifa zao.
Kwa upande wa jumuiya ya wanawake CUF taifa, amemteua Salama Masoud kuwa katibu mkuu wa jumuiya hiyo, badala ya Fatma Omary Kalembo kuwa na matatizo ya kiafya.
Aidha Profesa Lipumba amemuagiza Mkurugezi wa uchumi na fedha ambaye ndiye katibu wa bodi ya wadhamini, aitishe kikao cha dharula cha bodi ya wadhamini ili wapewe taarifa ya msimamo na mshauri wa usajili wa vyama vya siasa kuhusu mgogoro wa uongozi wa kitaifa ndani ya chama hicho siku ya Jumanne.
0 comments :
Post a Comment