SHILINGI YA EURO 2016 INA STORI YA WENYEJI FRANCE KUMTOA LASSANA DIARRA NA KUMWEKA MORGAN SCHNEIDERLIN!


Kiungo wa Manchester United Morgan Schneiderlin ameitwa Dakika za mwishoni kujiunga na Kikosi cha France ambao ndio Wenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya EURO 2016.
Jana ilikuwa Siku ya mwisho kwa Washiriki 24 wa Fainali za EURO 2016 kuwasilisha kwa UEFA Vikosi vyao vya Wachezaji 23 na France walilazimika kumchomoa Kiungo wa Marseille Lassana Diarra baada kuumia Goti na kumwita Schneiderlin.
Uteuzi huo wa Kiungo huyo wa Man United umefanywa na Kocha wa France Didier Deschamps ambae Siku za hivi karibuni amewapoteza Wachezaji kadhaa kutokana na maumivu na miongoni mwao ni Raphael Varane wa Real Madrid na Jeremy Mathieu wa Barcelona.
Kwenye EURO 2016, Wenyeji France wapo Kundi A pamoja na Romania, Albania na Switzerland.
France watafungua EURO 2016 hapo Juni 10 huko Stade de France, Paris kwa kucheza na Romania.
France - Kikosi UEFA EURO 2016:
Makipa: Benoît Costil (Rennes), Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Steve Mandanda (Marseille).
Mabeki: Lucas Digne (Roma), Patrice Évra (Juventus), Christophe Jallet (Lyon), Laurent Koscielny (Arsenal), Eliaquim Mangala (Manchester City), Samuel Umtiti (Lyon), Bacary Sagna (Manchester City), Adil Rami (Sevilla).
Viungo: Yohan Cabaye (Crystal Palace), Morgan Schneiderlin (Manchester United), N'Golo Kanté (Leicester City), Blaise Matuidi (Paris Saint-Germain), Paul Pogba (Juventus), Moussa Sissoko (Newcastle United).
Mafowadi: Kingsley Coman (Bayern München), André-Pierre Gignac (Tigres), Olivier Giroud (Arsenal), Antoine Griezmann (Atlético Madrid), Anthony Martial (Manchester United), Dimitri Payet (West Ham United)
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment