Umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Iringa CHASO na jumuiya ya vijana wa chama cha Demkorasia na maendeleo Chadema (BAVICHA) wameitaka serikali kuwarudisha chuoni wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) walioondolewa siku za hivi karibuni ili waweze kuendelea na masomo yao.
Wametoa kauli hiyo wakati wakizungumza na waandishi wa habari na kudai kuwa jambo lililofanywa na serikali ni ukiukwaji wa haki za binadamu hasusani haki ya kupata elimu.
Aidha wameonesha wasiwasi wao juu ya maisha ya wanafunzi hao kuondolewa chuoni hapo kwa madai kuwa Dodoma ni mji mdogo ukilinganisha na idadi ya wanafunzi walioondolewa huku wakiitaka serikali kubadilisha uamuzi na msimamo wake juu ya wanachuo hao.
Katika hatua nyingine wamewamemtaka waziri wa wizara ya elimu, sayansi na teknolojia Joyce Ndalichako kufuatilian suala hilo kwa ukaribu na kueleza kuwa mgomo wa walimu kuingia darasani hauhusiani na suala la kuwarudisha wanafunzi makwao na kwamba wanafunzi hawana kosa lolote.
Hata hivyo wanachuo hao pamoja na Bavicha wametoa msimamo wao endapo serikali itashindwa kutatua tatizo la wanafunzi hao.
Uamuzi wa kusimamishwa masomo kwa wanafunzi hao ulitolewa tangu Mei 25 mwaka huu jambo ambalo limepelekea hata wabunge wa upinzani kususia vikao huku wakitakiwa kuendelea kutekeleza majukumu yao hata kama wapo nje ya bunge.
0 comments :
Post a Comment