Ofisi ya
makamu wa rais inayoshughulikia muungano na mazingira imeanza kufanya tathmini
ya kiwango cha uharibifu wa mazingira kilichosababishwa na tetemeko la ardhi
lililotokea mkoani Kagera hivi karibuni lililosababisha vifo,majeruhi na
uharibifu wa miundombinu.
Hayo
yamesemwa na waziri wa sekta hiyo January Makamba, alipotembelea waathirika wa
tetemeko hilo akiwa na wataalam kutoka baraza la mazingira la taifa NEMC,
ambapo amesema watachunguza mfumo wa mazingira ulioathirika ili kujiridhisha
kama kuna uharibifu wa mazingira ulioweza kujitokeza kabla ya kufanya ukarabati
mpya.
Pamoja na
makamba kutembelea majeruhi katika hospitali ya mkoa wa Kagera na majeruhi
katika wilaya za Misenyi na hospitali ya Bukoba, lakini baadhi ya waathirika
wamelalamika kuchelewa kwa baadhi ya misaada, na kuomba kasi ya ugawaji
kuongezwa.
Makamba amesema
wizara yake imetoa wataalam kadhaa watakaotafiti namna vyanzo vya maji
vilivyoathirika, ikiwemo mifumo ya maji safi na taka ili kuzuia uwezekano wa
kuwepo kwa milipuko ya magonjwa inayoweza kutokea kutokana na miundombinu mingi
kuharibika wakati wa tetemeko hilo.
0 comments :
Post a Comment