Baada ya Lyon kukataa kumsajili Adebayor, kiungo huyu anafunguliwa mlango....

Klabu ya Lyon imejiondoa katika juhudi za kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal,Manchester City na Tottenham Emmanuel Adebayor.
Adebayor ambaye ni ajenti huru baada kuachiliwa na Crystal Palace alisafiri hadi mjini Lyon na kukutana na kocha Bruno Genesio siku ya Ijumaa.
Lakini klabu hiyo ya Ligue 1 haikufurahishwa na hatua za kumkosa mchezaji huyo kwa miezi miwili ya msimu huu ambapo ataichezea Togo katika kombe la mataifa ya bara Afrika.
Lyon imesema kuwa kushindwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kuiwakilisha Lyon wakati wa mechi za kimakundi za klabu bingwa Ulaya pia ni swala tete.
Vilabu vinafaa kutoa orodha za wachezaji
watakaoviwakilisha kufikia Septemba mosi huku mabadiliko yoyote yakikataliwa,hata iwapo mchezaji yupo huru, hadi pale raundi ya muondoano inapoanza.

Lyon ilisema katika taarifa yake kwamba
inafurahia kumsajili mshambuliaji mwengine Jean Phillipe Mateta baada ya Adebayor kusema kuwa angependa kuliwakilisha taifa lake katika kombe
la bara Afrika mapema 2017, hatua ambayo
ingemfanya kutochezea timu hiyo kwa kati ya mwezi mmoja hadi miwili.

Kombe la bara Afrika litafanyika nchini Gabon kati ya Januari 14 hadi Februari 5.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment