Hii ni habari iliyoripotiwa na kituo cha TBC, ambapo kijana Said Mamba (24) mkazi wa Mandewa, Manispaa ya Singida, amelazwa
hospitali baada ya kung’atwa sehemu ya ulimi wake na mwanamke waliyekuwa
wakinyonyana ndimi.
Mamba ambaye kwa sasa hawezi kuzungumza, aling’atwa Septemba 12, saa 3:30 usiku wa kumkia Sikukuu ya Idd el Hajj.
Alisema siku ya tukio alikutana na mwanamke huyo kwenye grosari
iliyopo eneo la Mandewa na baadaye mwanamama huyo alimwomba amsindikize
nyumbani kwake.
“Nilikubali kumsindikiza, tukiwa njiani aliniomba tufanye mapenzi.
Nilipokataa alinilazimisha na baada ya kuona sitaki aliomba tuagane kwa
kunyonyana ndimi, nilikubali ombi hilo,” alisema.
Mamba alisema wakati wakiendelea, mwanamke huyo alianza kumvua mkanda
wa suruali lakini alimzuia ndipo alipomng’ata ulimi na kuondoka na
kipande.
0 comments :
Post a Comment