Mchungaji mmoja wa kipentekoste aliingia bar moja hapo Dar ili ahudumiwe kinywaji.
Mhudumu alipofika kwenye meza yake Mchungaji alimuagiza kinywaji:
Mchungaji: nipe bia ya kilimanjaro ya baridi
Mhudumu kwa sababu ya mambo mengi alipofika kaunta akasahau kama aliagizwa bia ya kilimanjaro moto au baridi.
Alimrudia na kumuuliza
Mhudumu: Samahani Mchungaji, hivi uliniagiza bia ya kilimanjaro ya moto au baridi?
Mchungaji akafadhaika kwa vile mhudumu alimtambua kuwa ni mchungaji naye haraka akamjibu hivi:
Mchungaji: nimesema maji ya kilimanjaro baridi.
0 comments :
Post a Comment