Wahitimu, viongozi na wageni waliohudhuria Mahafali ya 32 ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mkoani Morogoro, waliingiwa na simanzi wakati mtoto, Tamar Aaron Mbogho (11), alipojitokeza na kupokea Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD), akimwakilisha mama yake Swai Sophia Faustin ambaye alifariki dunia miezi sita kabla ya kufika siku ya mahafali.
Tamar, mtoto pekee wa marehemu, ambaye baba yake mzazi ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, Aaron Mbogho alifika katika hafla hiyo akiwa ameambatana na ndugu zake kadhaa, tayari kwa ajili ya kupokea heshima hiyo kwa niaba ya mama yake.
Kwa mujibu wa Mbogho, mkewe Dk Sophia alifariki dunia Mei 21, 2016, wakati huo akiwa ameshahitimu masomo yake kikamilifu na alisema Tamar ni mtoto wa pekee wa Sophia.
“Alikuwa ni mmoja wa wahitimu waliopaswa kutunukiwa shahada hiyo kwa sababu tayari alishahitimu na kubakia muda wa mahafali, lakini bahati mbaya akafariki dunia kabla ya muda kuwadia,” alisema na kuongeza.
“Binti yetu alipenda kwenda kuchukua shahada ya mama yake na alisindikizwa na ndugu zake wa familia. Ameniambia malengo yake ni kusoma kwa bidii ili aweze kupata Shahada ya Udaktari wa Falsafa kama mama yake, ” alisema Mbogho.
Katika mahafali hayo yaliyofanyika juzi katika Kampasi ya Solomon Mahlangu, Mazimbu, wahitimu 61 walifuzu na kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments :
Post a Comment