Jumapili
Novemba 27 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliendelea na
ziara yake katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam akiwa na
lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
Akiwa
katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa alipita katika viunga vya Kata ya
Manzese na kutokea sehemu ambapo kula kilabu kinachouza pombe za
kienyeji huku watu waliokuwa eneo hilo wakionekana kuwa wamelewa kiasi
cha kutotambuana.
“Hii achana nayo kabisa ni moto wa kuotea mbali. Hebu niikate kidogo uone,” Mzee
aliyefahamika kwa jina la Mandela alisikika akimtambia Paul Makonda
huku akipiga funda la pomne hiyo ya kienyeji hali inayoonyesha kuwa
hakuwa akifahamu kuwa anayezungumza naye ni Mkuu wa Mkoa.
Baadaye
alienda eneo lenye vibanda vya chumba kimoja kimoja, amabavyo inaelezwa
kuwa ni madanguro ambayo hutumika kufanyika biashara ya ukahaba hadi
kwa wasichana wenye umri mdogo. Hata hivyo kila mlango aliojaribu
kugonga ulikuwa umefungwa na hakuna aliyeitika na kufungua mlango.
“Hawa wakijua watu wa serikali wanakuja hapa basi hufunga biashara zote, sasa na hapa wamefunga, si rahisi kumpata mtu,” alisikika kijana mmoja mwenyeji wa eneo hilo akisema.
Akizungumza
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Shule ya Msingi Tandale, Mkuu wa
Mkoa Paul Makonda alisema serikali inafanya mipango ya kupata wawekezaji
ili kununua eneo hilo la Uwanja wa Fisi na kuwalipa fidia wakazi wa
eneo hilo ili vibanda vyote vivunjwe na kujengwa vitegauchumi badala ya
kuliacha eneo hilo liharibu maisha ya vijana.
0 comments :
Post a Comment