Baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kwenye Mradi Wa Mabasi Ya Mwendokasi (DART), Waziri mkuu ameahidi haya


Waziri mkuu Kassim Majaliwa amekagua utendaji kazi kwenye mabasi ya mwendokasi yanayotoa huduma katika Jiji la Dar es Salaam na kubaini changamoto kadhaa ambazo amesema zitarekebishwa kadri mradi utakavyokuwa ukiendelea kutoa huduma.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa Kimara baada ya kumaliza ziara hiyo Waziri Mkuu amesema ameamua kufanya hivyo kwa kushtukiza ili kuangalia matumizi ya njia za mabasi yakoje na pia kuchunguza ni nmana gani abiria wanaelewa kuitumia huduma hiyo.

Mhe. Kassim Majaliwa amedai kuridhishwa na namna mradi huo  unavyofanya kazi huku akieleza kuwa serikali itaangalia namna ya kutatua baadhi ya kero za mradi huo ikiwa ni pamoja na kusimamia uboreshaji wa ukataji tiketi ili kuondoa usumbufu kwa abiria.
Aidha waziri mkuu amewataka watumiaji wa vyombo vingine vya moto kuacha mara moja kutumia njia ya magari ya mwendokasi huku akilitaka jeshi la polisi jijini humo hususani maaskari wanaofanya doria nyakati za usiku kupita njia ya fly over ili kuwaondoa watu wanaolala kwenye maeneno hayo kwa madai kuwa wananhatarisha usalama wa watumiaji wa njia hizo.
Kwa upande wake, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohammed Mpinga ambaye alifuatana na Waziri Mkuu katika ziara hiyo amepiga marufuku magari na pikipiki kutumia njia hiyo hata kama ni magari ya Serikali lengo likiwa ni kuondoa usumbufu usiokuwa wa lazima.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment