Baadhi ya wanahabari Mkoani Iringa wamelalamikia kitendo cha waajiri wao kupuuza suala la utoaji wa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi wao jambo linalodaiwa wengi wao kupoteza haki zao za msingi.
Wametoa malalamiko hayo wakati wakizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel aliyefanya ziara mkoani humo lengo likiwa ni kukagua shughuli mbalimbali zinazoendeshwa chini ya Wizara hiyo hatimaye kukutana na wanafani hao ili kuzungumza nao kuhusu kero zinazowakabili.
Wameeleza kuwa tatizo la ukosefu wa mikataba baina yao na waajiri limekuwa kikwazo kikubwa kinachopelekea baadhi yao kukata tama huku wakiitaka Wizara iangalie kwa umakini suala hilo na kuliingiza katika Sheria tarajiwa ya vyombo vya habari hapa nchini.
Wakiwasilisha maoni yao wanahabari hao akiwemo Leonard Frank amesema kuwa waandishi wengi wanategemea bahasha katika kuendesha maisha yao ya kila siku jambo linalopelekea kwa asilimia kubwa kuishi maisha duni huku wakiiomba serikali kukutana na wamiliki wa vyombo hivyo ili kutafuta suluhisho la tatizo hilo.
Akijibia malalamiko ya wanahabari katibu Mkuu wa wizara hiyo Olesante Gabriel amewataka wamiliki kutoa mikataba kwa wafanyakazi wao pasipo kusubiri sheria mpya ya vyombo hivyo huku akidai kuwa mkataba ni haki ya msingi kwa mfanyakazi yeyote.
0 comments :
Post a Comment