Wabunge wa vyama vya upinzani wametoka nje ya bunge kwa mara nyingine lengo likiwa ni kumpinga Naibu Spika Dk. Tulia Ackson kuendesha vikao vya Bunge na kuwaacha baadhi ya wabunge wa chama tawala wakiendelea na kikao hicho.
Taarifa kutoka Bungeni mjini Dodoma zinaeleza kuwa Mgomo huo umetokea Mei 31 mwaka huu majira ya asubuhi ambapo wabunge wote wa upinzani wamesusia kikao cha Bunge ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani na mhe. Naibu spika.
Wabunge hao wametoka nje ya bunge muda mfupi mara baada ya kusomwa dua ya kufungua kikao ambapo mgomo huo ni moja ya utekelezaji wa adhma ya upinzani waliotoa msimamo wao Mei 30 mwaka huu ya kuwa endapo kikao cha bunge kitaendeshwa na naibu spika wao watatoka nje kwa madai kuwa hawana imani naye.
Utekelezwaji wa kauli ya Mbowe umeanza rasmi Mei 31 mwaka huu wakati wakitekeleza adhma yao ya kususaia kikao chochote kitakachoeendeshwa na naibu spika, na hali ilikuwa kama ifuatavyo.
0 comments :
Post a Comment