Baadhi ya wananchi Mkoani Njombe wamezituhumu taasisi za umma kujihusisha na masuala ya rushwa jambo ambalo wamedai kuwa linapeleka kuzorota kwa utaoji wa huduma bora kwa wananchi wanapohitaji kupata huduma mbalimbalimbali katika ofisi hizo.
Wametoa malalamiko wakati wakizungumza na waandishi wa habari ambapo wameeleza kuwa baadhi ya maofisa wa taasisi hizo wamekuwa wakiwataka kutoa fedha ili kutimiziwa huduma wanazozihitaji ikiwa ni pamoja na kusainiwa mikataba kwenye taasisi za kifedha huku wakiiomba serikali kuangalia kwa upande wa pili suala hilo kwani linasababisha watu wengi kukosa haki zao za msingi.
Akijibia lawama hizo Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Njombe mhe. John Kapokolo ameeleza kuwa vitendo vya Rushwa ni kosa la jinai ambavyo hutendeka baina ya mtoa rushwa na mpokea rushwa na kuwahimiza wananchi wanaokutana na tatizo kama hilo kutoa taarifa mapema ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Miongoni mwa mambo yanayopingwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ni pamoja na rushwa, ubadhilifu, urasimu na upotevu wa mapato ya serikali huku akionesha kutokubaliana na vitu vinavyorudisha nyuma uchumi wa taifa.
0 comments :
Post a Comment