Watu nane wamefariki dunia katika tukio la kuchinjwa na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi katika mtaa wa Kibatini kata ya Mzizima jijini Tanga huku viongozi wa kata hiyo wakilitupia lawama jeshi la polisi mkoani hum kwa madai kuwa limeshindwa kuimarisha ulinzi katika maeneo hayo.
Wakizungumza na waandishi wa habari viongozi wa kata hiyo wamelilalikia jeshi la polisi mkoani humo kwa madai kuwa wameshindwa kuimarisha ulinzi na usalama wa raia ipasavyo jambo ambalo limepelekea wananchi hao kupoteza maisha ingawa askari wa jeshi hilo wameweka kambi katika eneo hilo.
Wakizungumza kuhusu mauaji hayo baadhi ya wananchi wa mtaa wa Kibatini wamedai kusikitishwa na matukio ya mauaji yanayotokea mkoani humo nakuiomba serikali kuimarisha ulinzi ili kunusuru uhai wa raia hao kwani hali iliyopo kwa sasa inatishia usalama wa wakazi hao.
Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Tanga Leonard Paul amewataja watu waliopoteza maisha katika tukio hilo kuwa ni Issa Hussein mwenye umri wa miaka 50, Nkola Hussein (40), Hamis Issa (20), Mwekidadi Hassani (70) ambaye ni mwenyekiti wa mtaa huo, Issa Ramadhani (25), Mahamudu (40), Kadri (25) na Salmu (35) ambao wameuwawa kwa kukatwa mapanga shingoni.
Hii ni mara ya pili wavamizi hao kufanya matukio ya kinyama kwenye mtaa huu, na kabla ya tukio la mauaji hayo ya kikatili wahalifu hao waliwahi kuvamia mtaa huo na kufanikiwa kuchinja kuku 40, ng’ombe 15 na Mbuzi 8 na tukio hilo limefanyika umbali wa kilometa 47 kutoka halmashauri ya jiji la Tanga.
Msikilize kamanda wa polisi Jijini Tanga Leonard Paul hapa chini:-
Msikilize kamanda wa polisi Jijini Tanga Leonard Paul hapa chini:-
0 comments :
Post a Comment