Hivi nini faida ya michepuko.,
hakuna cha mchepuko wa lami wala vumbi,mchepuko ni mchepuko tu.
Hutokuwa na amani ukiwa na mchepuko,utawaza kukamatwa tu masaa yote.
Ya nini presha aisee,kwanini usibaki njia kuu mbona maisha yanakuwa rahisi sana.Chagua unayempenda muweke na mfunze mwenza wako kuwa utakavyo..sasa kama wewe utakuwa unahangaika na kila chupi au wallet ipitayo tutaishi kweli.
kwanini uogopeshe ambao wanaingia kwenye ndoa waogope waone ni jela wanaingia,inaogopesha sana kama mnakaa baa mpaka saa kumi na una mke na familia au mume na watoto.
Kama unapenda kutoka kwanini usitoke na mwenza wako ,na kama hapendi basi toka ila wahi kurudi,usidhani hapendi unapokuwepo nyumbani hata kama ni mpiga kelele kiasi gani,bado anafurahia uwepo wako nyumbani.
tujifunze kuepusha baadhi ya magonjwa ya kujitakia,vifo vya bila kupangwa na mengineyo hatari
0 comments :
Post a Comment