Jeshi la polisi wilayani Iringa limetakiwa kuanzisha operesheni ya kufanya doria hususani nyakati za usiku ili kuwabaini watu wanaojihusisha na vitendo vya kikatili hususani ubakaji na mauaji.
Adefrida Mpete.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakati akizungumza na wanahabari kufuatia uwepo wa malalamiko ya baadhi ya wananchi mkoani humo juu ya matukio kama hayo huku wakiitupia lawama serikali pamoja na jeshi la polisi wilayani humo.
Akijibia malalamiko ya wananchi hao mkuu wa wilaya hiyo Richard Kasesela amesema kua vitendo vya ubakaji, ulawiti, mauaji na uhalifu mwingine ni miongoni mwa vitu visivyopaswa kufumbiwa macho katika jamii na hapa anazungumza.
Vitendo vya ubakaji ,ulawiti na mauaji vimekuwa vikijitokeza mara kwa mara katika maeneo mbalimbali nchini jambo linalopelekea wananchi wengi kuishi kwa wasiwasi na kupelekea kukwama kwa shughuli za kiuchumi na kimaendeleo.
Karibu kusikiliza ripoti ya Adefrida Mpete wa Starter fm Radio akiripoti hapa #JOSEPHKIPANGULABLOG.
0 comments :
Post a Comment