Baba yake Messi anahusika kwenye kesi ya kodi?


Mchezaji maarufu duniani Lionel Messi amesema hafahamu jambo lolote kwejye mikataba anayosaibi kwa sababu huwa hana utaratibu wa kusoma.
Kauli hii ya Lionel Messi inakuja wakati kesi yake ya ukwepaji kofi inatarajiwa kuendelea Jumanne ya leo, Katika kesi hiyo Messi na Baba yake Jorge Horacio wanatuhumiwa kukwepa kodi ya kiasi cha 4.1 million euros katika kipindi cha baina ya  2007 na  2009.
Kwa mujibu wa gazeti la Catalan la El Periodico, Messi alimwambia jaji mwaka 2013: “Namuamini baba yangu, ambaye anashughulikia biashara zangu zote. “Chochote anachoniambia nifanye, nafanya.”
Alipoulizwa kama huwa anasomaga mikataba yake kabla ya kusaini, nahodha huyo wa Argentina.
“Nasaini kila kitu lakini sijawahi kusoma mikataba.
“Sijui nini nasaini.”
Baada ya ratiba ya leo ya kesi Messi anatarajiwa kurudi kujiunga na timu yake ya taifa ya Argentina kwa ajili ya michuano ya Copa America inayotarajiwa kuanza tarehe 4, June.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment