Wengi tunafahamu kuwa Ace Hood alikuwa kwenye label ya We the Best Music Group inayosimamiwa na Dj Khaled pale Deff Jam Records.
Kubwa linalotrend kwa sasa ni kwanini msanii huyu wa muda mrefu kwenye hiyo Label hajawekwa kwenye project mpya ya Dj Khaled ile ya Major Key?.
Khaled amepiga stori na kipindi cha Morning Breakfast cha Power Fm huko Marekani na anasema kuwa baada ya Ace Hood kujitoa kwenye Label yake na kuanzisha Label nyingine inayokwenda kwa jina la Hood Nation hajawahi kuwaza mabaya juu yake na bado anamkubali kwa asilimia 100 hata kama akirudi kuomba kufanya naye tena kazi.
“Everybody makes their own decisions, but at the end of the day, we got love, I can’t speak for him, I don’t know what he’s thinking but at the end of the day, we bless him, we love him. I been with him from the birth of Ace Hood so I’ve supported him, and I’m always going to love him. If he ever needs me I’m here to support 100 percent.”
Hayo ni maneno ya Ace hoo yakielezea kuhusu kuendelea kumsapoti Ace Hood ingawa anasema hajui kuwa msanii huyo anafikiria nini kwa sasa lakini alikuwa naye tangu jina la Ace lilipoanza kukua.
Kwa upande wa Ace Hood ameonyeshwa kupendezwa na maneno ya Dj Khaled kwenye mahojiano hayo na kuongeza kuwa yeye anataka kuwapa watu uzoefu alioupata na alio nao kwa sasa.
Mwishowe pia Ace Hood alipost kwenye ukurasa wake wa Twitter maneno yasemayo If ONLY everything u said on BF club was the truth my brother.
Itizame Video ya Dj Khaled alipokuwa akihojiwa kwenye Power Breakfast pale Chini.
0 comments :
Post a Comment