Waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Mheshimiwa William Lukuvi anasema kuna utaratibu mpya unaotaraji kuanzishwa wa mfumo mpya wa kielektroniki utakaosimamia na kuratibu shughuli zote za kiardhi unaokwenda kwa jina la Intergrated Land Management Information System ambao utasaidia kuwafahamu maafisa ardhi ambao wanatumia ujanja mwingi kujinufaisha.
Kupitia mfumo huo, Serikali ya Tanzania imeingia mkataba na nchi ya Ufaransa ambapo tarehe 26 mwezi huu ndio utazinguliwa rasmi.
Asilimia kubwa ya maafisa ardhi nchini Tanzania ni wanyang'anyi na waporaji hii ni kwa mujibu wa Mheshimiwa William Lukuvi. Kupitia hilo Waziri Lukuvi anasema mpango mpya wa usimamizi wa ardhi saula hilo litakomeshwa na haki ya ardhi itasimamiwa.
Kwa upande wa nyumba za kupangishwa Waziri Lukuvi anasema vitaanzishwa vyama vya wapangaji kupitia mamlaka husika ambapo ikitokea mwenye nyumba anataka kuongeza kodi lazima awe na sababu za msingi ikiwemo kuangaliwa thamani ya nyumba na sio kujitakia tu.
0 comments :
Post a Comment