The Game kuachia albam mpya ya 1992 Septemba mwaka huu


Mkongwe wa muziki wa HihHop kutoka magharibi mwa mji wa America huko Los Angels Carlifonia, The Game ameamua kutangaza kuachia albam yake ya kumi Septemba mwaka huu kama Solo studio Album ambayo inajumuisha maisha yake ya muziki tangu mwaka 1992.

Hii ni albam inayojumuisha baadhi ya nyimbo zake ambazo pengine umewahi kuzisikia lakini hazikuwa kwenye albam kama Streets of Compton na Block Wars ambazo zilikuja kuingizwa kwenye albam mbili zilizokuwa kwenye mfumo wa Documentary 2 na Documentary 2.5.

Kufikia Septemba mwaka huu The Game anakuwa ameachia Project tano kubwa ambazo zote ni za faida na ni kitu anachojivunia.

Ngoma yake ya All Eyes aliyomshirikisha Jeremih ni kati ya ngoma ambazo ztakuwepo kwenye hiyo project yake mpya kwa kuwa ni  ya kwanza kwenye albam hiyo, na kwa mujibu wa CASH Machine Records ambako The Game amefanyia wimbo huo wanasema utakuwa umeachiwa rasmi Jumanne ijayo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment