Mpango wa Manji kuikodi Yanga umevunjika, sababu ziko hapa piaaa


Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ametangaza kujiuzulu kwenye nafasi yake hiyo ndani ya klabu hiyo.
Maamuzi hayo ya kushtukiza ya mwenyekiti huyo yamekuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu alipotangaza kutaka kuikodi timu hiyo kwa muda wa miaka kumi huku asilimia 75 za timu hiyo zikiingia kwake na kutoa asilimia 25 kwa timu hiyo kila mwaka.
Imedaiwa kuwa Manji ameamua kujiuzulu kwenye nafasi hiyo kutokana na baadhi ya watu kuonekana kuyapinga maamuzi hayo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Hilo linaelezwa kuwa pigo kubwa ndani ya Yanga kwani tayari wapinzani wao Simba wapo katika hatua za kufanya mabadiliko na hilo linatajwa kuwachanganya viongozi wa Yanga kwani inasemekana kuwa wamekuwa wakipishana katika ofisi za Manji zilizopo katika jengo la Quality Plaza wakimsihi abadilishe maamuzi yake.
“Kuna watu ndani ya Yanga wananufaika na migogoro inayotokea ndani ya Klabu,” amesema mwenyekiti msaidizi wa timu hiyo Clement Sanga.
Hata hivyo kuondoka kwa Manji kunaweza kukawa si pigo sana kwakuwa wengine kadhaa wanadaiwa kuitaka timu hiyo akiwemo mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi na tajiri namba moja Afrika, Aliko Dangote wa Nigeria.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment