Liverpool imeichapa Arsenal bao 4-3 kwenye mchezo wao wa kwanza wa Premier League iliopigwa kwenye dimba la Emirates Stadium.
Theo Walcott alianza kuifungia The Gunners bao la kwanza dakika ya 31ikiwa ni muda baada ya mkwaju wake wa penati kuokolewa na golikipa wa Liverpool.
Philippe Coutinho aliisawazishia Liverpool kwa mpira wa adhabu ndogo kabla ya Adam Lallana kufunga tena baada ya mapumziko.
Coutinho akafunga tena bao la pili kisha Sadio Mane akapachika bao la nne kabla ya Arsenal kupambana na kupata magoli mengine kupitia kwa Alex Oxlade-Chamberlain na Calum Chambers.
Rekodi 7 zilizowekwa kwenye mchezo wa Arsenal vs Liverpool
- Arsenal imekubali kichapo cha magoli manne kwenye mchezo wa ligi kwa mara ya kwanza tangu May 2009 (4-1 v Chelsea).
- Mechi inayozikutanisha Arsenal v Liverpool imeshuhudiwa wachezaji wake wakikosa penati nyingi zaidi kwenye historia ya Premier League.
- Mignolet ameokoa penati tano kati ya 11 alizokutana nazo kwenye Premier League, penati nyingi zaidi kuliko golikipa yeyote wa Liverpool.
- Walcott amefunga kwenye misimu 10 tofauti ya Premier League akiwa na Arsenal, Dennis Bergkamp ndiye anaeongoza kufunga katika misimu mingi (akiwa kafunga ndani ya misimu 11) akiwa na The Gunners.
- Magoli 13 kati ya 30 aliyofunga Philippe Coutinho kwenye mashindano yote akiwa na Liverpool, magoli hayo ameyafunga akiwa nje ya box.
- Arsenal imekuwa na wafungaji watatu tofauti raia England ndani mechi moja ya Premier League tangu October 1997 dhidi ya Barnsley (Parlour, Platt na Wright).
- Hii ni mara ya kwanza tangu 1954-54 kwenye ligi ya England kushuhudia vilabu viwili vya juu katika msimu uliopita vyote kupoteza mechi zao za ufunguzi.
0 comments :
Post a Comment