Waziri wa ardhi. nyumba na maendeleo ya makazi Mh.William Lukuvi amezitaka halmashauri za vijiji kuanza kupima na kumilikisha maeneo ambayo yameanza kuonekana kuwa na mwonekano wa miji ili kuepuka watu wanaojimilikisha na mwisho wa siku kuonekana wamenyang;anywa maeneo.
Akiongea kwenye kipindi cha Power Break Fast cha Clouds Fm Lukuvi nasemsa kuwa kasi ya serikali kuboresha miundombinu vijijini hususan kwenye sekta ya nishati ya umeme inafanya vijiji kukua na kuondokana na maisha ya kizamani hivyo serikali za vijiji zinatakiwa kufahamu hilo na kuweza kuchukua hatua stahiki mapema.
Waziri Lukuvi pia anasema wameandaa mpango maalum (Master Plan) wa kusimamia maeneo ya serikali na haki za ardhi na wameshaanza tayari kwa mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo kuangalia eneo lenye rasilimali muhimu na kuweza kufanya ujenzi utakaoleta faida kwa eneo na taifa kwa ujumla.
Sikiliza mahojiano haya kwa kubonyeza play hapo chini>>>>
0 comments :
Post a Comment