Hii imenifikia kutoka mafinga mkoani hapa Iringa tunaambiwa Familia moja inataka kuonana na viongozi wa serikali akiwemo mkuu wa mkoa wa Iringa bi. Amina Msenza au wizara ya maliasili na utalii kufuatia kutoa siri ya uvunaji
haramu wa misitu katika misitu ya Sao Hill na kutishiwa kutolewa uhai wao.Akizungumza na kituo cha redio Ebon Fm Iringa baba wa familia hiyo, Patrick Kinyunyu anasema amemuandikia barua mkuu wa wilaya, mkuu wa TAKUKURU Mafinga na meneja wa misitu ya Sao Hill kupata msaada lakini bado hajafanikiwa.
Familia hii yenye watu watano inasema imelazimika kwenda kuishi porini mara baada ya kuvamiwa mara mbili na kundi la watu, na kuwatishia kudhuru uhai wao.
Kwa upande wa serikali husika ya eneo walipokua wakiishi wahusika imeshutumiwa kwa kutowajali na kutokuchukua hatua stahiki kwa wahusika.
Ishu nzima ni kwamba kuna watu ambao wanakata magogo majira ya usiku kwenye msitu huo na kusafirisha usiku,kitendo hicho kilimuuma mzee huyo ndipo akaamua kuanza kutoa taarifa mahali husika.
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Joviki Kasonga anasema kwa sasa hawezi kuzungumza zaidi kwa masuala ya usalama.
0 comments :
Post a Comment