Nakuja Dar es Salaam wiki ijayo Kumpongeza Rais Magufuli na Kuendelea Kumsihi Aitimize ahadi Yake ya Kuniajiri ili Tuendelee Kutumbua Majipu,'Mrema'


Huyu ni Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha TLP na aliyekuwa mgombea Ubunge wa jimbo la Vunjo, Agustino Mrema anatarajia kusafiri kuja jijini Dar es salaam kwa lengo la kumpongeza Rais Magufuli na kumkumbusha ahadi aliyompa mwaka jana ya kumpatia kazi Serikalini.

Akizungumza kupitia kipindi cha Sun Rise kinachoruka kupitia Times fm, Mrema amempongeza Rais kwa jitihada za ukusanyaji kodi na kupambana na Ufisadi kwa nguvu.

“Tuweke itikadi pembeni Rais wa sasa anaweka juhudi katika kukusanya kodi, na mimi nilikuwa napiga nalo sana kelele hili swala, ila akipewa ushirikiano baada ya miaka mitano tutasheherekea mafanikio yake.

“Wiki ijayo natarajia kuja Dar, na nafikiri nitaonana na Rais kwanza nimpongeze alafu nimsisitize anipe nafasi kuna sehemu nazijua tuzisafishe, siwezi kusema mpaka nionane nae ndio nitamueleza”.

Mrema pia alijivunia rekodi yake ya uongozi katika Serikali ya Tanzania, kama kigezo kimoja wapo cha kumpatia ‘Chambirecho’ ya kupewa nafasi katika Serikali ya Magufuli.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment