Makonda atoa onyo kwa wafanyakazi hewa Dar es salaam {VIDEO}

Hali ya kutumbuana majipu kwa viongozi mbali mbali inaendelea na safari hii Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa kazi ya kutafuta watumishi hewa katika manispaa za jiji la Dar es Salaam bado inaendelea
baada kubaini njia chafu wanazotumia watumishi hewa hao.

Akizungumza leo na waandishi habari ,Makonda amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ni kioo kwa nchi hivyo jitihada zinaendelea ya kutafuta na kazi hiyo itafanywa sekta kwa sekta.

Amesema kuwa Wakuu wa Wilaya katika jiji la Dar es Salaam hakuna kufanya kazi yeyote mpaka wamelize kutafuta watumishi hewa kwa kutumia malipo ya watumishi kutoka taasisi za fedha (Pay Row).

Makonda amesema idadi ya watumishi hewa 71 aliowasilisha kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –Tamisemi, Georgre Simbachawene  ni ndogo katika  jiji la Dar es Salaam hivyo kazi lazima iwe endelevu.

Amesema kuwa watumishi Hewa hawawezi wakawa wanalipwa mshahara huku wanaofanya kazi kwa moyo mmoja wanajisikia  vibaya hivyo ni lazima watafutwe na wachukuliwe hatua na vyombo vya dola.

Mkuu Mkoa amesema kuwa kati ya watumishi hewa 71 ni watumishi 34 hewa wamefunguliwa mashitaka katika mahakama mbalimbali kutokana kuchukua fedha wasioifanyia kazi.

Tizama video:-
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment