Mwanadada ambaye ni msanii wa kike kutoka Tanzania anayetamba na kibao cha mahaba niue, Maua Sama amesema kuchelewa kutoka kwa video ya Mahaba niue ni kutaka kufanya video nzuri ambayo itadumu kwa muda
mrefu katika playlist za vituo mbali mbali vya Tv na sio kukimbilia kutafuta kutoka zaidi kama wasanii wengine wanavyofanya.Akipiga stori na mtangazaji wa kituo cha redio, Nuru fm Iringa, Roger Magoha, Maua kazungumzia pia kuhusu ujio wake mpya baada ya mahaba niue kwa kusema kuwa kuna vitu vingi zaidi vizuri vinavyokuja ingawa hakutaka kuweka wazi zaidi.
Maua pia kasema kuwa ni vizuri kwa wasanii wachanga kuweka jitihada zaidi katika kutafuta mafanikio bila kufuata njia za mkato. Aliongeza pia kusema kuwa hata yeye amepitia mengi mpaka kufikia hapa alipo kwahiyo ni vizuri kutokua na moyo wa kukata tamaa.
0 comments :
Post a Comment