Jana April 20, 2016 klabu ya Simba kupitia kwa mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyo Haji Manara walitangaza maamuzi ambayo hayakutarajiwa na wengi
ya kumfungia beki wake wa pembeni Hassan Kessy kwa kosa la kuigharimu timu.“Kessy juzi ameigharimu timu hatujui kwa makusudi au bahati mbaya, Kessy ameigharimu timu kwa kucheza rafu mbaya tena yenye nia mbaya kwa Edward Christopher kwa kumpandishia mguu kichwani kwa makusudi, licha ya kuoneshwa kadi nyekundu na refa na kukosa mechi mbili, Simba inamuongezea adhabu na kumfungia mechi 5” >>> Haji Manara
0 comments :
Post a Comment