Jana April 22 2016 ilikuwa ni kikao cha Bunge la 11 mjini Dodoma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwasilisha hotuba yake ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2016/2017.
Akiongea na Waandishi wa habari nje ya bunge, Dodoma Kiongozi wa upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema ‘Hatutashiriki mjadala wa kibunge hadi tutakapopata rejea mpya ya muundo wa Serikali, Pili tatizo la bajeti za Serikali kufanywa kinyume cha sheria, n Serikali yenyewe inakiri tatizo hili‘ ;-Freeman Mbowe
‘Mwisho kabisa lazima muelewe, Bunge ni chombo cha Umma, sio mali ya mtu yoyote, tunapokuwa katika Bunge, kazi zinafanyika ndani ya Bunge na nje ya Bunge, kuna nia ya kuzuia mjadala unaojadili madhambi yanayofanyika katika Serikali yetu‘ ;–Freeman Mbowe
‘Kama Serikali ya Rais Magufuli inajiamini, iruhusu mjadala huu uwe wa wazi na wa haki, sisi tunataka tumsaidie Rais kwasababu yeye amesema anataka Serikali ya uwazi, aturuhusu sisi tuielezee dunia madhara yaliyofanyika katika Serikali ya Nne na ya Tano ambayo huwenda kuna mengine hayajui‘ ;-Freeman Mbowe
Kilichopo kwamba kua watu waliyopewa kazi maalum ya kurekodi matukio ya Bunge yote yanayofaa kufikishiwa Wananchi na hayo matukio ndio wanapewa Waandishi wa habari ila hakuna tena utaratibu kama wa zamani kwamba kila mwandishi anaweza kurekodi kwa Camera yake chochote anachoona ni habari.
April 22 2016 vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wametangaza kutokuchangia bajeti zote zinazoendelea ndani ya bunge hadi pale Serikali itakaporekebisha vipengele vinavyo bana uhuru wa bunge kama vile kuruhusu urushwaji wa matangazo ya moja kwa moja na vyombo vingine kurekodi bila vizuizi.
0 comments :
Post a Comment