Hili ndilo jno kubwa la Nyangumi lilioonekana msimu huu!


Hii inashangaza kidogo, ni taarifa ihusuyo Jino kubwa la nyangumi kumepatikana ufukweni nchini Australia na kuwa uthibitisho wa kwanza kwamba nyangumi wakubwa
hatari sana waliishi mbali na Amerika.
Mkusanyaji wa visukuku Murray Orr alipata jino hilo lenye urefu wa sentimeta 30 (inchi 12) ufukweni Beaumaris Bay karibu na mji wa Melbourne mwezi Februari.
Alilikabidhi kwa makumbusho ya Victoria, ambayo yalianza kulionesha kwa umma Alhamisi.
Inakadiriwa kwamba nyangumi mwenye jino hilo aliishi zaidi ya miaka milioni tano iliyopita. Alitoka kwa aina ya nyangumi ambao siku hizi hawapatikani duniani.
Nyangumi hao wanaaminika kuwa watangulizi wa nyangumi wakubwa wa sasa wajulikanao kwa Kiingereza kama "sperm whales".

Hadi kupatikana kwa jino hilo Beaumaris, visukuku vya nyangumi wakubwa vilikuwa vinapatikana pwani ya magharibi ya mabara ya Amerika Kusini na Amerika Kaskazini.
Makavazi hiyo imesema nyangumi mwenye jino hilo huenda alikuwa na urefu wa mita 18 na uzani wa tani 40
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment