Msanii wa Bongo Fleva, Cyril Kamikaze amekutwa na ishu nzima ya msala wa kumgonga trafiki na kuwekwa ndani
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika ambacho ni mmoja wa mashuhuda,trafiki ameweza kufahamika kwa jina la Afande Francis, tukio hilo lililokuwa kama sinema ya kivita lilijiri wiki iliyopita majira ya saa 5:00 asubuhi jirani na Hospitali ya Magomeni, Dar, wakati trafiki huyo akitekeleza majukumu yake ya kuongoza magari barabarani.
Ilidaiwa kuwa, trafiki huyo alimsimamisha Cyril ambaye alimpuuza na kumgonga.
“Alichokifanya Cyril ni unyama, kama alijijua ana makosa angesimama tu na kumsikiliza.
Afande Francis anayedaiwa kugonga na Cyril na kusababishiwa majeraha.
“Kwanza alimgonga, yule trafiki akajihami kwa kurukia juu ya gari kwa mbele (kwenye boneti), akazidi kukimbiza gari ili ammwage barabarani.
“Hata hivyo, mashuhuda walimsifu sana yule trafiki maana kama asingekuwa yupo fiti kwa kujiokoa, basi angekufa,” kilisema chanzo hicho.
Kwa upande wake trafiki huyo alipoombwa na Ijumaa Wikienda kuelezea mkasa huo, huku akiwa na masikitiko makubwa alisema, hadi sasa haamini kama yupo hai kutokana na ujasiri mkubwa alioutumia kujiokoa, kwa kuwa kila anapojiuliza Cyril alikusudia nini, anakosa jibu.
“Niliona gari ndogo lenye ‘tinted’ nzito linakuja, nikaamua kulisimamisha, cha ajabu likasimama lakini baada ya kuona nakaribia kulifikia akaliondoa kwa kasi na kunigonga. Ndipo nikachukua bodaboda kulikimbiza hadi kwenye Kona ya Kwa-Shehe Yahya.
….Baadhi ya majeraha madogo aliyoyapata afande huyo.
“Pale pia hakusimama, akavuka upande wa pili, kulikuwa na gari la driving school, nikaliamuru ‘lim-block’. Nikashuka kwenye bodaboda na kusimama mbele ya gari lake.
“Badala ashuke, ndiyo kwanza akalitoa gari kwa kasi huku akiniburuza na kunigonga,” alisema Afande Francis.
Alisema baada ya kuona hivyo, alilazimika kujirusha kwenye boneti ya gari hilo ili kunusuru uhai wake, lakini Cyril hakujali kwani aliendelea kuendesha kwa kasi akiliyumbisha ili afande huyo aishiwe nguvu na kuanguka barabarani.
Gari lake likiwa chini ya ulinzi.
“Lengo lake lilikuwa animwage kisha anikanyage na gari ili nife, alipoona nimeshikilia wepa, akawa anazichezesha nikose pa kushika, ikanilazimu nipige ngumi kioo cha gari, mkono ukapita ndani nikamshika ndo akasimamisha gari.
Alikuwa akikimbia kwa sababu gari lake limekutwa vibali vimeisha na hakuwa na leseni,” aliongeza Afande Francis.
Kufuatia ishu hiyo, trafiki huyo anaendelea vizuri japokuwa ana majeraha madogo mkononi huku msanii huyo akishikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Magomeni kwa jalada la kesi namba MAG/TR/RB/110/206 SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI NA KUKATAA AMRI HALALI 13/4/2016 akisubiri kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa msala huo ambao umemkalia vibaya.
Chanzo:Globalpublishers
0 comments :
Post a Comment