Baada ya kufunga bao akiwa Man United, Zlatan kayasema haya...


Zlatan Ibrahimovic anaamini kwamba kuna kitu kizuri anakiona mbele ya Manchester United baada ya kufunga goli lake aina ya bicycle-kick, ukiwa ni mchezo wake wa kwanza tangu asajilie klabuni hapo.
Ibrahimovic, 34, aliunganisha krosi ya Antonio Valencia kwa umaridadi wa hali juu, katika mchezo ambao United waliwafunga Galatasaray mabao 5-2.
Lakini baadaye Waturuki hao walikuja kwa kasi na kumaliza kipindi cha kwanza wakiongoza kwa magoli 2-1, shukarni ziende kwao Sinan Gumus na Bruma.
Lakini Manchester United ambayo ilionekana kubadilika walikuja na kasi ya aina yake kipindi cha pili na kufunga magoli mawili ya haraka-haraka yaliyofungwa na Wayne Rooney kabla ya Marouane Fallaini na Juan Mata kukamilisha karamu ya magoli
Na sasa mshambuliaji huyo mwenye asili ya Sweden anaamini kwamba anaona kitu kizuri kinakuja siku za usoni klabuni hapo, ikiwa ni pamoja na kuhusishwa kwa ujio wa Pogba kwa kitita cha paundi mil 100 kutoka Juventus.
“Kuna kitu kinakuja siku za usoni, utakuwa ni mwaka wa aina yake klabuni hapa,” amesema. “Ngoja tuseme tu kwamba kama Pogba pia atakuja, kutakuwa na utamu wa kutosha hapa.
Ameongeza: “Nitaisaidia timu kwa kadri nitakavyoweza na nitafanya kila zuri kuhakikisha kwamba timu inasonga mbele, ikiwa ni pamoja na kutenegeneza nafasi za magoli na kufunga magoli pia.”
Ibrahimovic aliongoza safu ya ushambuliaji ya Man United kipindi cha kwanza akiwa mbele ya Rooney huku Anthony Martial na Henrikh Mkhitaryan wakitokea pembeni.
Vilevile wakali wengine waliongia kipindi cha pili kama vile Marcus Rashford, Ashley Young Jesse Lingard walionekana kuwa moto wa kuotea mbali baada ya kuiongoza United kupata ushindi mnono.
Rooney alisawazisha bao baada ya kuunganisha mpira kwa umaridadi wa hali ya juu uliopigwa na Valencia cross kabla ya Rashford kusababisha penati na Rooney tena kuiweka kimiani.
Valencia baadaye tena alitoa krosi murua iliyounganishwa kwa kichwa na Marouane Fellaini drifted na Mata, ambaye aliuzwa na Mourinho wakati akiwa Chelsea, alifunga goli la mwisho kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Michael Carrick.
Bastian Schweinsteiger hakucheza kutokana na taarifa zilizoenea kueleza kwamba, Mourinho amedai hayupo kwenye mipango yake.
Jose Mourinho anasemaje:
“Kama wachezaji hawakuwa kwenye mipango yangu, nisingeweza kuwapa hata dakika moja. Nisingeweza pia kuwajumuisha kwenye kikosi changu
“Kikosi kina ushindani mkubwa, kina umuhimu mkubwa kuelekea msimu mpya.
“Tuna michezo 38 kwenye ligi ya Englanda, tuna uwezekano wa kuwa na michezo 15 katika mashindano ya Europa, jumlisha na makombe ya ndani, tutakuwa na takriban michezo 60. Hivyo kwa idadi hiyo ya mechi hatuwezi kufanikiwa kwa kuchezesha wachezaji 11 tu.
“Unapokuwa kikosini unatakwa kutambua kwamba, kikosi ni muhimu zaidi kuliko mchezaji mmoja-mmoja, klabu ni muhimu kuliko sisi sote, na ili kuwa kwenye kikosi lazima uwe tayari kwa haya yote, kucheza ama kutocheza, kucheza sana, kucheza mara cheche, kucheza dakika moja, kutokuchaguliwa. Kila kitu ni sehemu ya maisha ya kikosi hiki.”
Chanzo: ShaffihDauda
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment