Picha: Baada ya Koffi Olomide kuachiwa huru amewashukuru Mashabiki wake


Tukirudi nyuma kidogo tunaona Koffi Olomide Alikamatwa Jumanne July 26 2016 nyumbani kwake Kinshasa kwa tuhuma za kumshambulia dancer wake wa kike wakati wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata Nairobi na baadaye ikawa imeripotiwa kuwa 
amehukumiwa kwenda jela miezi 18 na adhabu hiyo kutajwa kuwa haitakuwa na faini.

Taarifa zilizoripotiwa ni kwamba Koffi Olomide kaachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha siku mbili kati ya miezi 18 aliyohukumiwa awali.
 BBC imeripoti kuwa kuachiwa kwa koffi Olomide kumekuja baada ya Mahakama ya Kinshasa kusema kuwa hawakuona sababu za kutosha za kuhukumiwa kwa Koffi Olomide kutokana na tukio alilofanya JKIA.

Pamoja na baadhi ya vyombo vya habari Afrika kuripoti kwamba Koffi alihukumiwa kifungo cha miezi 18 jela , Promoter wake wa nchini  Kenya Jules Nsana amekanusha madai hayo  na kusema  kesi dhidi ya Koffi ilikuwa bado iko kwenye uchunguzi na kwamba baada ya uchunguzi wamebaini hakuna ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani Koffi Olomide.

Promoter Jules amesema Olomide alimpigia simu akamtaka aombe msamaha kwa wakenya wote kwa niaba yake

Habari mpya ni kuwa Koffi amewashukuru mashabiki wake kwa kuendelea kumpa moyo na kutomchukia kwa aliyoyafanya

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Koffi ameandika ujumbe huu wenye lugha ya kiCongo ambao unamaanisha shukrani,""À la maison en Famille. .... Merci est un mot trop simple. Ce que je souhaiterais exprimer est au-dessus de cela. Je suis à la fois touché et reconnaissant pour le soutien indéfectible que vous m'avez apporté, je ne pourrai jamais assez vous remercier #BétonArmé #Agbada (I'm home Family. Thanks .... is too simple a word. What I would like to express is above that. I am both humbled and grateful for the unwavering support you have given me, I can never thank you enough #BétonArmé #Agbada)"

Hii ni picha iliyoambatana na ujumbe huo
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment