Haya ni matano ya kufahamu kabla ya fainali ya Euro 2016 Ureno vs Ufaransa


Kwa sasa kinachosubiriwa kwa hamu ni mchezo wa fainali ya michuano ya Euro 2016 kati ya timu ya taifa ya Ureno dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa, huu ni mchezo ambao utachezwa katika uwanja wa Stade de France wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 80000. Kabla ya mchezo huo utakaochezwa July 10 2016 hivi ni vitu vitano vya kufahamu.
1- Ureno wanaingia kucheza mchezo wa fainali ya Euro 2016, wakiwa na rekodi ya kufungwa mechi zao 10 za mwisho mfululizo dhidi ya Ufaransa.
2- Ureno na Ufaransa wamecheza jumla ya mechi 24, Ureno amewahi kumfungaUfaransa mara 5 na kutoka sare mara 1, huku akiwa ameruhusu kufungwa mara 18.
3- Mara ya mwisho Ureno kumfunga Ufaransa ilikuwa ni April 26 1975 kwa goli 2-0 katika mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki, yaani imepita miaka 41.
4- Hii itakuwa fainali ya 17 kwa Cristiano Ronaldo kucheza katika maisha yake ya soka, ameshinda jumla ya fainali 11 kati ya 16 ambazo tayari ameshacheza.
5- Antoine Griezmann ndio mchezaji anayeshikilia rekodi ya ufungaji bora wa muda wote katika hatua ya mtoano, akiwa kafunga jumla ya goli 5.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment