Baada ya Yanga kushindwa kupata pointi tatu katika mchezo wake wa
tatu mfululizo kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika ikiwa ni
hatua ya makundi, mkufunzi mkuu wa timu hiyo Hans van Pluijm amesema
kikibwa kilicho wakosesha ushindi kwenye mchezo dhidi ya Medeama ni
kushindwa kutukia nafasi zilizopatikana kwenye mchezo huo.
“Nilijua kabla kwamba Medeama ni timu nzuri wanacheza mpira wa nguvu,
ukipata nafasi unatakiwa kuitumia vema na kama tungezitumia nafasi zetu
tungeshinda mechi”, amesema kocha huyo wa Yanga ambaye tayari
amekiongoza kikosi chake kwenye mechi tatu za Kundi A na kuambulia
pointi moja pekee na kushuhudia timu yake ikiburuza mkia katika kundi
hilo.
“Kwa ujumla timu imefanya kazi kubwa, lakini muda mwingi tulitumia
mipira mirefu, hatukucheza mchezo wetu wa pasi na hii ilisababishwa na
tension kubwa kwenye timu yetu”.
“Kama usipocheza kwa style yako, inakuwa ni vigumu kutengeneza nafasi
na kufunga hapo presha inazidi kuwa kubwa lakini morali ya timu
kupambana ilikuwa ni nzuri. Tulitarajia kushinda hata ungiangalia
mazoezi yetu ya wiki hii yalikuwa ni kushambulia na kufunga magoli
lakini soka ni mchezo wa makosa ukishindwa kufunga unakuwa kwenye wakati
mgumu”.
“Kwa upande mwingine tungepoteza mechi hii dakika mbili au tatu za
mwisho, Medeama walipata nafasi moja na wao wakaipoteza nafasi hiyo
pia”.
0 comments :
Post a Comment