Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour
Party (TLP), Augustino Mrema, amefurahia uteuzi wake wa kuwa Mwenyekiti
wa Bodi ya Taifa ya Parole huku akieleza Rais John Magufuli amelipa
ahadi yake aliyomwahidi wakati wa kampeni ya uchaguzi Mkuu.
Jana Rais Magufuli alifanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa
taasisi mbalimbali za serikali huku akimteua Mrema kuwa mwenyekiti wa
bodi hiyo katika kipindi cha miaka mitatu.
Akihojiwa jana kwa njia ya simu, Mrema alisema anamshukuru Rais
Magufuli kwa kumpatia nafasi hiyo na ameoonyesha ni mtu ambaye
anatekeleza ahadi zake.
“Rais alivyokuja Vunjo katika kampeni zangu aliwaambia wannachi
wamchague Mrema kwa kuwa ni jembe na akawaambia wasiponichagua atanipa
kazi watu wakajua ni utapeli wa kisiasa sasa wajue kuwa Rais huwa
anaishi kwa ahadi na amenipa kazi ambayo ninaijua,” alisema Mrema
0 comments :
Post a Comment