Aliyekuwa mgombea Urais kupitia Ukawa Mh.Edward Lowassa amezungumzia mambo kadhaa yanayoendelea ndani ya nchi ya Tanzania hususan Bungeni ikiwemo ile ishu ya wabunge kujifunga bandeji midomoni.
Mh Lowassa alikuwepo kwenye kipindi cha Funguka cha Azam Tv, na kusema kuwa kuhusu ishu ya Ukawa kumpinga Naibu Spika, tatizo limetokana na Spika Ndugai kuwa na hali mbaya ya afya, huku akisema kuwa anamfahamu Ndugai ni mtu makini sana’
Lowassa anasema wabunge wake anawaelewa vizuri na atazungumza nao ingawa bajeti imepita bila kupitishwa na wabunge wa upinzani ambapo kitu hicho si salama kwa Demokrasia.
0 comments :
Post a Comment