"Wivu haihusiani na mapenzi yangu na Vanessa", Jux

 
Jux ni msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni mpenzi wa Vanessa Mdee amefunguka na kusema kuwa wimbo wake mpya ‘Wivu’ ambao unafanya vizuri kwa sasa hajaimba kwa ajili ya mpenzi wake Vanessa Mdee,mbali ameimba wimbo huo kutokana na hisia kwani jambo hilo linawakuta wengi ambao wanapendana kweli katika mahusiano yao ya kila siku.
Jux akizungumza kwenye kipindi cha ENEWZ ya EATV alidai kwenye mapenzi kama hakuna wivu kati ya wawili wapendanao hapo kunakuwa hakuna mapenzi ya kweli kati yao kwani wivu ndiyo ishara ya upendo wa kweli.
“Wimbo wa Wivu ni matukio ya kimapenzi ambayo yanatokea kwa watu wengi ila siyo kama nimejiimbia mimi, unajua kabla sijarekodi wimbo ule tukiwa studio niliwauliza wakina Bob Manecky na wengine jamanii mnadhani ‘idea’ hii inaweza kuwa sawa ndipo hapo wakaniambia ni wazo zuri kwani kwenye mapenzi bila uwepo wa wivu kuna kuwa hakuna mapenzi ya kweli, ndiyo hapo nikajua kumbe suala hili linawagusa watu wengi” alisema Jux.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment