Haya hapa madhara ya Shisha na kauli ya kudhibiti matumizi yake Tanzania...


Kuna watu ambao hajafahamu madhara kadha wa kadha yanayosababishwa na uvutaji wa Shisha, katika vitu muhimu unatakiwa kuvijua ambavyo mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametusogezea ni pamoja na hizi athari  kuu tisa zinazopatikana kwa mtu yeyote ambaye anatumia shisha ikiwemo matatizo ya kiafya na kisaikolojia kwa mujibu wa TFDA .

1. Shisha inasababisha kansa ya koo

2.Shisha inaleta kansa ya mapafu

3. Shisha ni chanzo cha watoto njiti

4. Ni chanzo cha ugonjwa wa moyo

5. Inapunguuza uwezo wa kufikiri na kufanya uso kuwa na makunyanzi

6. Inasababisha kupunguza nguvu za tendo la ndoa

7. Inasababisha mtu kusinziasinzia bila sababu 

8. Watengenezaji hawana utaalamu wa vipimo  

9. Inapoteza nguvu kazi ya taifa kutokana na vijana wengi kujihusisha na uvutaji huo

‘Mimi nasema kwenye mkoa wangu nikikukuta unafanya biashara ya shisha tutakukuta segerea, nawaagiza wakuu wa wilaya na ma RPC kuanzia jumatatu ya wiki ijayo maeneo yote yanayofanya biashara hiyo yawe yamefungwa’
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment